Hosea 2:20
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nitakuposa kwa uaminifu, nawe utamkubali Bwana.
Hosea 2:20 in English
Hosea 2:20 · Berean Standard Bible
And I will betroth you in faithfulness, and you will know the LORD.”
Context
18Katika siku ile nitafanya Agano kwa ajili yao
na wanyama wa kondeni, na ndege wa angani,
na viumbe vile vitambaavyo ardhini.
Upinde, upanga na vita,
nitaondolea mbali katika nchi,
ili kwamba wote waweze kukaa salama. 19Nitakuposa uwe wangu milele;
nitakuposa kwa uadilifu na haki,
kwa upendo na huruma. 20Nitakuposa kwa uaminifu,
nawe utamkubali Bwana. 21“Katika siku ile nitajibu,”
asema Bwana,
“nitajibu kwa anga,
nazo anga zitajibu kwa nchi; 22nayo nchi itajibu kwa nafaka,
divai mpya na mafuta,
navyo vitajibu kwa Yezreeli.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.