Hosea 11:10
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Watamfuata Bwana; atanguruma kama simba. Wakati angurumapo, watoto wake watakuja wakitetemeka kutoka magharibi.
Hosea 11:10 in English
Hosea 11:10 · Berean Standard Bible
They will walk after the LORD; He will roar like a lion. When He roars, His children will come trembling from the west.
Context
8“Efraimu, ninawezaje kukuacha?
Ee Israeli, ninawezaje kukutoa?
Nitawezaje kukutendea kama Adma?
Nitawezaje kukufanya kama Seboimu?
Moyo wangu umegeuka ndani yangu,
huruma zangu zote zimeamshwa. 9Sitatimiza hasira yangu kali,
wala sitageuka na kumharibu Efraimu.
Kwa kuwa mimi ndimi Mungu,
wala si mwanadamu,
Aliye Mtakatifu miongoni mwenu.
Sitakuja kwa ghadhabu. 10Watamfuata Bwana;
atanguruma kama simba.
Wakati angurumapo,
watoto wake watakuja wakitetemeka
kutoka magharibi. 11Watakuja wakitetemeka
kama ndege wakitoka Misri,
kama hua wakitoka Ashuru.
Nitawakalisha katika nyumba zao,”
asema Bwana. 12Efraimu amenizunguka kwa uongo,
nyumba ya Israeli kwa udanganyifu.
Naye Yuda ni mkaidi dhidi ya Mungu,
hata kinyume cha yule mwaminifu Aliye Mtakatifu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.