Hosea 10:13
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Lakini mmepanda uovu, mkavuna ubaya, mmekula tunda la udanganyifu. Kwa sababu mmetegemea nguvu zenu wenyewe na wingi wa mashujaa wenu,
Hosea 10:13 in English
Hosea 10:13 · Berean Standard Bible
You have plowed wickedness and reaped injustice; you have eaten the fruit of lies. Because you have trusted in your own way and in the multitude of your mighty men,
Context
11Efraimu ni mtamba wa ngʼombe aliyefundishwa
ambaye hupenda kupura,
hivyo nitamfunga nira
juu ya shingo yake nzuri.
Nitamwendesha Efraimu,
Yuda lazima alime,
naye Yakobo lazima avunjavunje
mabonge ya udongo. 12Jipandieni wenyewe haki,
vuneni matunda ya upendo usio na kikomo,
vunjeni ardhi yenu isiyolimwa;
kwa kuwa ni wakati wa kumtafuta Bwana,
mpaka atakapokuja
na kuwanyeshea juu yenu haki. 13Lakini mmepanda uovu,
mkavuna ubaya,
mmekula tunda la udanganyifu.
Kwa sababu mmetegemea nguvu zenu wenyewe
na wingi wa mashujaa wenu, 14mngurumo wa vita utainuka dhidi ya watu wako,
ili kwamba ngome zako zote zitaharibiwa:
kama Shalmani alivyoharibu Beth-Arbeli katika siku ile ya vita,
wakati mama pamoja na watoto wao
walipotupwa kwa nguvu ardhini. 15Ndivyo itakavyotokea kwako, ee Betheli,
kwa sababu uovu wako ni mkuu.
Siku ile itakapopambazuka,
mfalme wa Israeli ataharibiwa kabisa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.