Native Bible

Hebrews 9:18 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Hii ndiyo sababu hata lile agano la kwanza halikuweza kutekelezwa pasipo damu.

Hebrews 9:18 in English

Hebrews 9:18 · Berean Standard Bible

That is why even the first covenant was not put into effect without blood.

Context

16Kwa habari ya wosia,* ni muhimu kuthibitisha kifo cha yule aliyeutoa, 17kwa sababu wosia huwa na nguvu tu wakati mtu ameshakufa; kamwe hauwezi kutumika wakati yule aliyeuandika bado yuko hai. 18Hii ndiyo sababu hata lile agano la kwanza halikuweza kutekelezwa pasipo damu. 19Mose alipotangaza kila amri kwa watu wote, alichukua damu ya ndama na ya mbuzi, pamoja na maji, sufu nyekundu na matawi ya mti wa hisopo, akanyunyizia kile kitabu na watu wote. 20Alisema, “Hii ndiyo damu ya agano, ambalo Mungu amewaamuru kulitii.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.