Waebrania 9:19
Hebrews 9:19 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mose alipotangaza kila amri kwa watu wote, alichukua damu ya ndama na ya mbuzi, pamoja na maji, sufu nyekundu na matawi ya mti wa hisopo, akanyunyizia kile kitabu na watu wote.
Hebrews 9:19 in English
Hebrews 9:19 · Berean Standard Bible
For when Moses had proclaimed every commandment of the law to all the people, he took the blood of calves and goats,* along with water, scarlet wool, and hyssop, and sprinkled the scroll and all the people,
Context
17kwa sababu wosia huwa na nguvu tu wakati mtu ameshakufa; kamwe hauwezi kutumika wakati yule aliyeuandika bado yuko hai. 18Hii ndiyo sababu hata lile agano la kwanza halikuweza kutekelezwa pasipo damu. 19Mose alipotangaza kila amri kwa watu wote, alichukua damu ya ndama na ya mbuzi, pamoja na maji, sufu nyekundu na matawi ya mti wa hisopo, akanyunyizia kile kitabu na watu wote. 20Alisema, “Hii ndiyo damu ya agano, ambalo Mungu amewaamuru kulitii.” 21Vivyo hivyo alinyunyizia damu hiyo kwenye ile hema pamoja na kila kifaa kilichotumika ndani yake kwa taratibu za ibada.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.