Native Bible

Hebrews 9:16 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kwa habari ya wosia,* ni muhimu kuthibitisha kifo cha yule aliyeutoa,

Hebrews 9:16 in English

Hebrews 9:16 · Berean Standard Bible

In the case of a will,* it is necessary to establish the death of the one who made it,

Context

14Basi ni zaidi aje damu ya Kristo, ambaye kwa Roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na waa, itatusafisha dhamiri zetu kutokana na matendo yaletayo mauti, ili tupate kumtumikia Mungu aliye hai! 15Kwa sababu hii Kristo ni mpatanishi wa agano jipya, ili kwamba wale walioitwa waweze kupokea ile ahadi ya urithi wa milele: kwa vile yeye alikufa awe ukombozi wao kutoka kwa dhambi walizozitenda chini ya agano la kwanza. 16Kwa habari ya wosia,* ni muhimu kuthibitisha kifo cha yule aliyeutoa, 17kwa sababu wosia huwa na nguvu tu wakati mtu ameshakufa; kamwe hauwezi kutumika wakati yule aliyeuandika bado yuko hai. 18Hii ndiyo sababu hata lile agano la kwanza halikuweza kutekelezwa pasipo damu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.