Waebrania 10:14
Hebrews 10:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
kwa sababu kwa dhabihu moja amewafanya kuwa wakamilifu milele wale wote wanaotakaswa.
Hebrews 10:14 in English
Hebrews 10:14 · Berean Standard Bible
because by a single offering He has made perfect for all time those who are being sanctified.
Context
12Lakini huyu kuhani akiisha kutoa dhabihu moja kwa ajili ya dhambi kwa wakati wote, aliketi mkono wa kuume wa Mungu. 13Tangu wakati huo anangoja mpaka adui zake wawekwe chini ya miguu yake, 14kwa sababu kwa dhabihu moja amewafanya kuwa wakamilifu milele wale wote wanaotakaswa. 15Pia Roho Mtakatifu anatushuhudia kuhusu jambo hili. Kwanza anasema: 16“Hili ndilo Agano nitakalofanya nao
baada ya siku hizo, asema Bwana.
Nitaziweka sheria zangu mioyoni mwao,
na kuziandika katika nia zao.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.