Habakuki 3:8
Habakkuk 3:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ee Bwana, uliikasirikia mito? Je, ghadhabu yako ilikuwa dhidi ya vijito? Je, ulighadhibikia bahari ulipoendesha farasi wako na magari yako ya ushindi?
Habakkuk 3:8 in English
Habakkuk 3:8 · Berean Standard Bible
Were You angry at the rivers, O LORD? Was Your wrath against the streams? Did You rage against the sea when You rode on Your horses, on Your chariots of salvation?
Context
6Alisimama, akaitikisa dunia;
alitazama, na kuyafanya mataifa yatetemeke.
Milima ya zamani iligeuka mavumbi
na vilima vilivyozeeka vikaanguka.
Njia zake ni za milele. 7Niliona watu wa Kushani katika dhiki,
na makazi ya Midiani katika maumivu makali. 8Ee Bwana, uliikasirikia mito?
Je, ghadhabu yako ilikuwa dhidi ya vijito?
Je, ulighadhibikia bahari
ulipoendesha farasi wako
na magari yako ya ushindi? 9Uliufunua upinde wako
na kuita mishale mingi.
Uliigawa dunia kwa mito; 10milima ilikuona ikatetemeka.
Mafuriko ya maji yakapita huko;
vilindi vilinguruma
na kuinua mawimbi yake juu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.