Habakuki 2:3
Habakkuk 2:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa kuwa ufunuo huu unasubiri wakati uliokubalika; unazungumzia mambo ya mwisho, na kamwe hautakosea. Iwapo utakawia, wewe usubiri; kwa hakika utakuja na hautachelewa.
Habakkuk 2:3 in English
Habakkuk 2:3 · Berean Standard Bible
For the vision awaits an appointed time; it testifies of the end and does not lie. Though it lingers, wait for it, since it will surely come and will not delay.*
Context
1Nitasimama katika zamu yangu,
na kujiweka mwenyewe juu ya maboma;
nitatazama nione atakaloniambia,
na ni jibu gani nitakalotoa kuhusu lalamiko hili. 2Kisha Bwana akajibu:
“Andika ufunuo huu,
na ukaufanye wazi juu ya vibao,
ili mpiga mbiu akimbie nao. 3Kwa kuwa ufunuo huu unasubiri wakati uliokubalika;
unazungumzia mambo ya mwisho,
na kamwe hautakosea.
Iwapo utakawia, wewe usubiri;
kwa hakika utakuja na hautachelewa. 4“Tazama, amejaa majivuno;
anavyovitamani si vya unyofu:
lakini mwenye haki ataishi kwa imani yake: 5hakika mvinyo humsaliti;
ni mwenye kiburi na hana amani.
Kwa sababu ni mlafi kama kuzimu
na kama kifo kamwe hatosheki;
anajikusanyia mataifa yote
na kuchukua watu wote mateka.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.