Habakuki 2:13
Habakkuk 2:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Je, Bwana Mwenye Nguvu Zote hakuonyesha kwamba kazi ya wanadamu ni mafuta tu kwa ajili ya moto, na kwamba mataifa yanajichosha bure?
Habakkuk 2:13 in English
Habakkuk 2:13 · Berean Standard Bible
Is it not indeed from the LORD of Hosts that the labor of the people only feeds the fire, and the nations weary themselves in vain?
Context
11Mawe ya kuta yatapiga kelele,
na mihimili ya kazi ya mbao itarudisha mwangwi wake. 12“Ole wake yeye ajengaye mji kwa kumwaga
damu na kuusimamisha mji kwa uhalifu! 13Je, Bwana Mwenye Nguvu Zote hakuonyesha
kwamba kazi ya wanadamu ni mafuta tu kwa ajili ya moto,
na kwamba mataifa
yanajichosha bure? 14Kwa kuwa dunia itajazwa na maarifa ya utukufu wa Bwana,
kama maji yaifunikavyo bahari. 15“Ole wake yeye awapaye jirani zake kileo,
akiimimina kutoka kwenye kiriba
cha mvinyo mpaka wamelewa,
ili apate kutazama miili yao iliyo uchi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.