Native Bible

Habakkuk 2:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

“Ole wake yeye ajengaye mji kwa kumwaga damu na kuusimamisha mji kwa uhalifu!

Habakkuk 2:12 in English

Habakkuk 2:12 · Berean Standard Bible

Woe to him who builds a city with bloodshed and establishes a town by iniquity!

Context

10Umefanya shauri la maangamizi ya watu wengi, ukiaibisha nyumba yako mwenyewe, na kupotewa na maisha yako. 11Mawe ya kuta yatapiga kelele, na mihimili ya kazi ya mbao itarudisha mwangwi wake. 12“Ole wake yeye ajengaye mji kwa kumwaga damu na kuusimamisha mji kwa uhalifu! 13Je, Bwana Mwenye Nguvu Zote hakuonyesha kwamba kazi ya wanadamu ni mafuta tu kwa ajili ya moto, na kwamba mataifa yanajichosha bure? 14Kwa kuwa dunia itajazwa na maarifa ya utukufu wa Bwana, kama maji yaifunikavyo bahari.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.