Mwanzo 8:16
Genesis 8:16 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Toka ndani ya safina, wewe na mkeo na wanao na wake zao.
Genesis 8:16 in English
Genesis 8:16 · Berean Standard Bible
“Come out of the ark, you and your wife, along with your sons and their wives.
Context
14Katika siku ya ishirini na saba ya mwezi wa pili dunia ilikuwa imekauka kabisa. 15Ndipo Mungu akamwambia Noa, 16“Toka ndani ya safina, wewe na mkeo na wanao na wake zao. 17Utoe nje kila aina ya kiumbe hai aliye pamoja nawe: Ndege, wanyama na viumbe vyote vitambaavyo juu ya ardhi, ili wakazae, na kuongezeka na kuijaza tena dunia.” 18Kwa hiyo Noa akatoka nje pamoja na mkewe, wanawe na wake zao.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.