Native Bible

Genesis 6:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Hivi ndivyo utakavyoitengeneza: Safina iwe na urefu wa dhiraa 300,* upana wake dhiraa hamsini* na kimo chake dhiraa thelathini.*

Genesis 6:15 in English

Genesis 6:15 · Berean Standard Bible

And this is how you are to build it: The ark is to be 300 cubits long, 50 cubits wide, and 30 cubits high.*

Context

13Kwa hiyo Mungu akamwambia Noa, “Nitawaangamiza watu wote, kwa kuwa dunia imejaa ukatili kwa sababu yao. Hakika mimi nitaangamiza watu pamoja na dunia. 14Kwa hiyo jitengenezee safina kubwa kwa mbao za mvinje, tengeneza vyumba ndani yake na uipake lami ndani na nje. 15Hivi ndivyo utakavyoitengeneza: Safina iwe na urefu wa dhiraa 300,* upana wake dhiraa hamsini* na kimo chake dhiraa thelathini.* 16Itengenezee paa na umalizie safina kwa kuacha nafasi ya dhiraa moja* juu. Weka mlango ubavuni mwa safina, na uifanye ya ghorofa ya chini, ya kati na ya juu. 17Nitaleta gharika ya maji juu ya nchi ili kuangamiza uhai wote chini ya mbingu, kila kiumbe chenye pumzi ya uhai ndani yake. Kila kitu juu ya nchi kitaangamia.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.