Native Bible

Genesis 6:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kwa hiyo jitengenezee safina kubwa kwa mbao za mvinje, tengeneza vyumba ndani yake na uipake lami ndani na nje.

Genesis 6:14 in English

Genesis 6:14 · Berean Standard Bible

Make for yourself an ark of gopher wood;* make rooms in the ark and coat it with pitch inside and out.

Context

12Mungu akaona jinsi dunia ilivyoharibika, kwa maana watu wote duniani walikuwa wameharibu njia zao. 13Kwa hiyo Mungu akamwambia Noa, “Nitawaangamiza watu wote, kwa kuwa dunia imejaa ukatili kwa sababu yao. Hakika mimi nitaangamiza watu pamoja na dunia. 14Kwa hiyo jitengenezee safina kubwa kwa mbao za mvinje, tengeneza vyumba ndani yake na uipake lami ndani na nje. 15Hivi ndivyo utakavyoitengeneza: Safina iwe na urefu wa dhiraa 300,* upana wake dhiraa hamsini* na kimo chake dhiraa thelathini.* 16Itengenezee paa na umalizie safina kwa kuacha nafasi ya dhiraa moja* juu. Weka mlango ubavuni mwa safina, na uifanye ya ghorofa ya chini, ya kati na ya juu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.