Mwanzo 6:16
Genesis 6:16 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Itengenezee paa na umalizie safina kwa kuacha nafasi ya dhiraa moja* juu. Weka mlango ubavuni mwa safina, na uifanye ya ghorofa ya chini, ya kati na ya juu.
Genesis 6:16 in English
Genesis 6:16 · Berean Standard Bible
You are to make a roof * for the ark, finish its walls a cubit from the top,* place a door in the side of the ark, and build lower, middle, and upper decks.
Context
14Kwa hiyo jitengenezee safina kubwa kwa mbao za mvinje, tengeneza vyumba ndani yake na uipake lami ndani na nje. 15Hivi ndivyo utakavyoitengeneza: Safina iwe na urefu wa dhiraa 300,* upana wake dhiraa hamsini* na kimo chake dhiraa thelathini.* 16Itengenezee paa na umalizie safina kwa kuacha nafasi ya dhiraa moja* juu. Weka mlango ubavuni mwa safina, na uifanye ya ghorofa ya chini, ya kati na ya juu. 17Nitaleta gharika ya maji juu ya nchi ili kuangamiza uhai wote chini ya mbingu, kila kiumbe chenye pumzi ya uhai ndani yake. Kila kitu juu ya nchi kitaangamia. 18Lakini Mimi nitaweka Agano langu na wewe, nawe utaingia ndani ya Safina, wewe pamoja na mke wako, wanao na wake zao.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.