Mwanzo 45:23
Genesis 45:23 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hivi ndivyo vitu alivyotuma kwa baba yake: punda kumi waliochukua vitu vizuri vya Misri, punda wake kumi waliobeba nafaka, mikate na mahitaji mengine ya safari.
Genesis 45:23 in English
Genesis 45:23 · Berean Standard Bible
And he sent to his father the following: ten donkeys loaded with the best of Egypt, and ten female donkeys loaded with grain and bread and provisions for his father’s journey.
Context
21Hivyo wana wa Israeli wakafanya hivyo. Yosefu akawapa magari ya kukokotwa, kama Farao alivyoagiza, pia akawapa mahitaji kwa ajili ya safari yao. 22Kila mmoja mavazi mapya, lakini Benyamini akampa shekeli 300* za fedha, na jozi tano za nguo. 23Hivi ndivyo vitu alivyotuma kwa baba yake: punda kumi waliochukua vitu vizuri vya Misri, punda wake kumi waliobeba nafaka, mikate na mahitaji mengine ya safari. 24Akaagana na ndugu zake walipokuwa wakiondoka, akawaambia, “Msigombane njiani!” 25Basi wakatoka Misri na kufika kwa baba yao Yakobo katika nchi ya Kanaani.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.