Mwanzo 43:3
Genesis 43:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Lakini Yuda akamwambia, “Mtu yule alituonya kwa msisitizo, ‘Hamtauona uso wangu tena mpaka mje na ndugu yenu.’
Genesis 43:3 in English
Genesis 43:3 · Berean Standard Bible
But Judah replied, “The man solemnly warned us, ‘You will not see my face again unless your brother is with you.’
Context
1Wakati huu njaa ilikuwa bado ni kali mno katika nchi. 2Hivyo wakati walikuwa wamemaliza kula nafaka yote waliyoileta kutoka Misri, Yakobo baba yao akawaambia, “Rudini Misri mkatununulie chakula kingine zaidi.” 3Lakini Yuda akamwambia, “Mtu yule alituonya kwa msisitizo, ‘Hamtauona uso wangu tena mpaka mje na ndugu yenu.’ 4Kama utakubali ndugu yetu aende pamoja nasi, tutakwenda kuwanunulia chakula. 5Lakini ikiwa hutamruhusu aende, hatutakwenda, kwa sababu mtu yule alituambia, ‘Hamtauona uso wangu tena mpaka mje pamoja na ndugu yenu.’ ”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.