Mwanzo 43:4
Genesis 43:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kama utakubali ndugu yetu aende pamoja nasi, tutakwenda kuwanunulia chakula.
Genesis 43:4 in English
Genesis 43:4 · Berean Standard Bible
If you will send our brother with us, we will go down and buy food for you.
Context
2Hivyo wakati walikuwa wamemaliza kula nafaka yote waliyoileta kutoka Misri, Yakobo baba yao akawaambia, “Rudini Misri mkatununulie chakula kingine zaidi.” 3Lakini Yuda akamwambia, “Mtu yule alituonya kwa msisitizo, ‘Hamtauona uso wangu tena mpaka mje na ndugu yenu.’ 4Kama utakubali ndugu yetu aende pamoja nasi, tutakwenda kuwanunulia chakula. 5Lakini ikiwa hutamruhusu aende, hatutakwenda, kwa sababu mtu yule alituambia, ‘Hamtauona uso wangu tena mpaka mje pamoja na ndugu yenu.’ ” 6Israeli akauliza, “Kwa nini mkaniletea taabu hii kwa kumwambia yule mtu mlikuwa na ndugu mwingine?”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.