Native Bible

Genesis 41:45 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Farao akamwita Yosefu Safenath-Panea, pia akampa Asenathi binti Potifera, kuhani wa mji wa Oni,* kuwa mke wake. Ndipo Yosefu akaitembelea nchi yote ya Misri.

Genesis 41:45 in English

Genesis 41:45 · Berean Standard Bible

Pharaoh gave Joseph the name Zaphenath-paneah,* and he gave him Asenath daughter of Potiphera, priest of On,* to be his wife. And Joseph took charge of all the land of Egypt.

Context

43Akampandisha katika gari lake la farasi kama msaidizi wake, watu wakatangulia wakishangilia, wakisema, “Fungueni njia!” Ndivyo Farao alivyomweka Yosefu kuwa msimamizi wa nchi yote ya Misri. 44Kisha Farao akamwambia Yosefu, “Mimi ni Farao, lakini pasipo neno lako, hakuna mtu mwenye ruhusa kuinua mkono au mguu katika nchi yote ya Misri.” 45Farao akamwita Yosefu Safenath-Panea, pia akampa Asenathi binti Potifera, kuhani wa mji wa Oni,* kuwa mke wake. Ndipo Yosefu akaitembelea nchi yote ya Misri. 46Yosefu alikuwa na miaka thelathini alipoingia katika utumishi wa Farao mfalme wa Misri. Naye Yosefu akatoka mbele ya Farao akasafiri katika nchi yote ya Misri. 47Katika ile miaka saba ya neema nchi ilizaa mazao kwa wingi sana.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.