Mwanzo 41:47
Genesis 41:47 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Katika ile miaka saba ya neema nchi ilizaa mazao kwa wingi sana.
Genesis 41:47 in English
Genesis 41:47 · Berean Standard Bible
During the seven years of abundance, the land brought forth bountifully.
Context
45Farao akamwita Yosefu Safenath-Panea, pia akampa Asenathi binti Potifera, kuhani wa mji wa Oni,* kuwa mke wake. Ndipo Yosefu akaitembelea nchi yote ya Misri. 46Yosefu alikuwa na miaka thelathini alipoingia katika utumishi wa Farao mfalme wa Misri. Naye Yosefu akatoka mbele ya Farao akasafiri katika nchi yote ya Misri. 47Katika ile miaka saba ya neema nchi ilizaa mazao kwa wingi sana. 48Yosefu akakusanya chakula chote kilichozalishwa katika ile miaka saba ya neema nchini Misri, akakihifadhi katika ghala za miji. Katika kila mji kulihifadhiwa chakula kilichozalishwa katika mashamba yaliyouzunguka mji huo. 49Yosefu alihifadhi nafaka nyingi, mfano wa mchanga wa bahari, ilikuwa nyingi mno kiasi kwamba walishindwa kuweka kumbukumbu kwa sababu akiba ilizidi sana kupita kipimo.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.