Mwanzo 41:4
Genesis 41:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wale ngʼombe wabaya na waliokonda wakawala wale saba wazuri na wanono. Kisha Farao akaamka.
Genesis 41:4 in English
Genesis 41:4 · Berean Standard Bible
And the cows that were sickly and thin devoured the seven sleek, well-fed cows. Then Pharaoh woke up,
Context
2wakati ngʼombe saba, wazuri na wanono, walitokea mtoni wakajilisha kwenye matete. 3Baada yao ngʼombe wengine saba, wabaya na waliokonda, wakatokea mtoni Naili wakasimama kando ya wale wanono ukingoni mwa mto. 4Wale ngʼombe wabaya na waliokonda wakawala wale saba wazuri na wanono. Kisha Farao akaamka. 5Farao akaingia usingizini tena akaota ndoto ya pili: Akaona masuke saba ya nafaka, yenye afya na mazuri, yanakua katika bua moja. 6Baadaye, masuke mengine saba yakachipua, yakiwa membamba yaliyonyaushwa na upepo wa mashariki.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.