Mwanzo 41:2
Genesis 41:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
wakati ngʼombe saba, wazuri na wanono, walitokea mtoni wakajilisha kwenye matete.
Genesis 41:2 in English
Genesis 41:2 · Berean Standard Bible
when seven cows, sleek and well-fed, came up from the river and began to graze among the reeds.
Context
1Baada ya miaka miwili kamili kupita, Farao aliota ndoto: Tazama alikuwa amesimama kando ya Mto Naili, 2wakati ngʼombe saba, wazuri na wanono, walitokea mtoni wakajilisha kwenye matete. 3Baada yao ngʼombe wengine saba, wabaya na waliokonda, wakatokea mtoni Naili wakasimama kando ya wale wanono ukingoni mwa mto. 4Wale ngʼombe wabaya na waliokonda wakawala wale saba wazuri na wanono. Kisha Farao akaamka.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.