Native Bible

Genesis 41:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Baada yao ngʼombe wengine saba, wabaya na waliokonda, wakatokea mtoni Naili wakasimama kando ya wale wanono ukingoni mwa mto.

Genesis 41:3 in English

Genesis 41:3 · Berean Standard Bible

After them, seven other cows, sickly and thin, came up from the Nile and stood beside the well-fed cows on the bank of the river.

Context

1Baada ya miaka miwili kamili kupita, Farao aliota ndoto: Tazama alikuwa amesimama kando ya Mto Naili, 2wakati ngʼombe saba, wazuri na wanono, walitokea mtoni wakajilisha kwenye matete. 3Baada yao ngʼombe wengine saba, wabaya na waliokonda, wakatokea mtoni Naili wakasimama kando ya wale wanono ukingoni mwa mto. 4Wale ngʼombe wabaya na waliokonda wakawala wale saba wazuri na wanono. Kisha Farao akaamka. 5Farao akaingia usingizini tena akaota ndoto ya pili: Akaona masuke saba ya nafaka, yenye afya na mazuri, yanakua katika bua moja.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.