Native Bible

Genesis 4:22 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Pia Sila alikuwa na mtoto wa kiume aliyeitwa Tubali-Kaini ambaye alifua vifaa vya aina mbalimbali vya shaba na chuma. Naama alikuwa dada wa Tubali-Kaini.

Genesis 4:22 in English

Genesis 4:22 · Berean Standard Bible

And Zillah gave birth to Tubal-cain, a forger of every implement of bronze and iron. And the sister of Tubal-cain was Naamah.

Context

20Ada akamzaa Yabali ambaye ni baba wa wale walioishi katika mahema na kufuga wanyama. 21Kaka yake aliitwa Yubali, aliyekuwa baba wa wote wapigao zeze na filimbi. 22Pia Sila alikuwa na mtoto wa kiume aliyeitwa Tubali-Kaini ambaye alifua vifaa vya aina mbalimbali vya shaba na chuma. Naama alikuwa dada wa Tubali-Kaini. 23Lameki akawaambia wake zake, “Ada na Sila nisikilizeni mimi; wake wa Lameki sikieni maneno yangu. Nimemuua mtu kwa kunijeruhi, kijana mdogo kwa kuniumiza. 24Kama Kaini atalipizwa kisasi mara saba, basi Lameki itakuwa mara sabini na saba.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.