Mwanzo 38:3
Genesis 38:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
akapata mimba, akamzaa mwana, ambaye alimwita Eri.
Genesis 38:3 in English
Genesis 38:3 · Berean Standard Bible
So she conceived and gave birth to a son, and Judah named him Er.
Context
1Wakati ule, Yuda akawaacha ndugu zake, akaenda kuishi na Hira Mwadulami. 2Huko Yuda akakutana na binti wa Kikanaani aitwaye Shua, akamwoa na akakutana naye kimwili, 3akapata mimba, akamzaa mwana, ambaye alimwita Eri. 4Akapata mimba tena, akamzaa mwana na kumwita Onani. 5Akamzaa mwana mwingine tena, akamwita Shela. Huyu alimzalia mahali paitwapo Kezibu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.