Mwanzo 38:16
Genesis 38:16 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Pasipo kutambua kwamba alikuwa mkwe wake, akamwendea kando ya njia na kumwambia, “Njoo sasa, nikutane na wewe kimwili.” Yule mkwewe akamuuliza, “Utanipa nini nikikutana nawe kimwili?”
Genesis 38:16 in English
Genesis 38:16 · Berean Standard Bible
Not realizing that she was his daughter-in-law, he went over to her and said, “Come now, let me sleep with you.” “What will you give me for sleeping with you?” she inquired.
Context
14alivua mavazi yake ya ujane, akajifunika kwa shela ili asifahamike, akaketi kwenye mlango wa Enaimu, ambao upo njiani kuelekea Timna. Akafanya hivyo kwa sababu aliona kwamba, ingawa Shela amekua, lakini alikuwa hajakabidhiwa kwake kuwa mkewe. 15Yuda alipomwona alifikiri ni kahaba, kwa sababu alikuwa amefunika uso wake. 16Pasipo kutambua kwamba alikuwa mkwe wake, akamwendea kando ya njia na kumwambia, “Njoo sasa, nikutane na wewe kimwili.”
Yule mkwewe akamuuliza, “Utanipa nini nikikutana nawe kimwili?” 17Akamwambia, “Nitakutumia mwana-mbuzi kutoka kundi langu.”
Akamuuliza, “Utanipa kitu chochote kama amana mpaka utakapompeleka?” 18Akamuuliza, “Nikupe amana gani?”
Akamjibu, “Pete yako na kamba yake pamoja na fimbo iliyo mkononi mwako.” Kwa hiyo akampa vitu hivyo kisha akakutana naye kimwili, naye akapata mimba yake.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.