Mwanzo 38:15
Genesis 38:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Yuda alipomwona alifikiri ni kahaba, kwa sababu alikuwa amefunika uso wake.
Genesis 38:15 in English
Genesis 38:15 · Berean Standard Bible
When Judah saw her, he thought she was a prostitute because she had covered her face.
Context
13Tamari alipoambiwa, “Baba mkwe wako yuko njiani kwenda Timna kukata kondoo wake manyoya,” 14alivua mavazi yake ya ujane, akajifunika kwa shela ili asifahamike, akaketi kwenye mlango wa Enaimu, ambao upo njiani kuelekea Timna. Akafanya hivyo kwa sababu aliona kwamba, ingawa Shela amekua, lakini alikuwa hajakabidhiwa kwake kuwa mkewe. 15Yuda alipomwona alifikiri ni kahaba, kwa sababu alikuwa amefunika uso wake. 16Pasipo kutambua kwamba alikuwa mkwe wake, akamwendea kando ya njia na kumwambia, “Njoo sasa, nikutane na wewe kimwili.”
Yule mkwewe akamuuliza, “Utanipa nini nikikutana nawe kimwili?” 17Akamwambia, “Nitakutumia mwana-mbuzi kutoka kundi langu.”
Akamuuliza, “Utanipa kitu chochote kama amana mpaka utakapompeleka?”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.