Mwanzo 38:18
Genesis 38:18 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Akamuuliza, “Nikupe amana gani?” Akamjibu, “Pete yako na kamba yake pamoja na fimbo iliyo mkononi mwako.” Kwa hiyo akampa vitu hivyo kisha akakutana naye kimwili, naye akapata mimba yake.
Genesis 38:18 in English
Genesis 38:18 · Berean Standard Bible
“What pledge should I give you?” he asked. She answered, “Your seal and your cord, and the staff in your hand.” So he gave them to her and slept with her, and she became pregnant by him.
Context
16Pasipo kutambua kwamba alikuwa mkwe wake, akamwendea kando ya njia na kumwambia, “Njoo sasa, nikutane na wewe kimwili.”
Yule mkwewe akamuuliza, “Utanipa nini nikikutana nawe kimwili?” 17Akamwambia, “Nitakutumia mwana-mbuzi kutoka kundi langu.”
Akamuuliza, “Utanipa kitu chochote kama amana mpaka utakapompeleka?” 18Akamuuliza, “Nikupe amana gani?”
Akamjibu, “Pete yako na kamba yake pamoja na fimbo iliyo mkononi mwako.” Kwa hiyo akampa vitu hivyo kisha akakutana naye kimwili, naye akapata mimba yake. 19Tamari akaondoka, akavua shela yake akavaa tena nguo zake za ujane. 20Wakati ule ule, Yuda akamtuma rafiki yake Mwadulami apeleke yule mwana-mbuzi ili arudishiwe amana yake kutoka kwa yule mwanamke, lakini yule rafiki yake hakumkuta yule mwanamke.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.