Mwanzo 38:19
Genesis 38:19 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Tamari akaondoka, akavua shela yake akavaa tena nguo zake za ujane.
Genesis 38:19 in English
Genesis 38:19 · Berean Standard Bible
Then Tamar got up and departed. And she removed her veil and put on her widow’s garments again.
Context
17Akamwambia, “Nitakutumia mwana-mbuzi kutoka kundi langu.”
Akamuuliza, “Utanipa kitu chochote kama amana mpaka utakapompeleka?” 18Akamuuliza, “Nikupe amana gani?”
Akamjibu, “Pete yako na kamba yake pamoja na fimbo iliyo mkononi mwako.” Kwa hiyo akampa vitu hivyo kisha akakutana naye kimwili, naye akapata mimba yake. 19Tamari akaondoka, akavua shela yake akavaa tena nguo zake za ujane. 20Wakati ule ule, Yuda akamtuma rafiki yake Mwadulami apeleke yule mwana-mbuzi ili arudishiwe amana yake kutoka kwa yule mwanamke, lakini yule rafiki yake hakumkuta yule mwanamke. 21Akawauliza watu wanaoishi mahali pale, “Yuko wapi yule kahaba wa mahali pa kuabudia miungu aliyekuwa kando ya barabara hapa Enaimu?”
Wakamjibu, “Hajawahi kuwepo mwanamke yeyote kahaba wa mahali pa kuabudia miungu hapa.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.