Native Bible

Genesis 34:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Oaneni na sisi, tupeni binti zenu, nanyi mchukue binti zetu.

Genesis 34:9 in English

Genesis 34:9 · Berean Standard Bible

Intermarry with us; give us your daughters, and take our daughters for yourselves.

Context

7Basi wana wa Yakobo walikuwa wamerudi kutoka mashambani mara tu waliposikia kilichotokea. Walikuwa wamejawa na huzuni na ghadhabu, kwa sababu Shekemu alikuwa amefanya jambo la aibu katika Israeli kwa kukutana kimwili na binti wa Yakobo, kitu ambacho hakingepasa kufanyika. 8Lakini Hamori akawaambia, “Moyo wa mwanangu Shekemu umeelekea kwa binti yenu. Tafadhali mpeni awe mke wake. 9Oaneni na sisi, tupeni binti zenu, nanyi mchukue binti zetu. 10Mwaweza kuishi katikati yetu, nchi ni wazi kwenu. Ishini ndani yake, fanyeni biashara humu na mjipatie mali.” 11Kisha Shekemu akamwambia baba yake Dina pamoja na ndugu zake, “Na nipate kibali machoni penu, nami nitawapa chochote mtakachosema.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.