Mwanzo 34:8
Genesis 34:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Lakini Hamori akawaambia, “Moyo wa mwanangu Shekemu umeelekea kwa binti yenu. Tafadhali mpeni awe mke wake.
Genesis 34:8 in English
Genesis 34:8 · Berean Standard Bible
But Hamor said to them, “My son Shechem longs for your daughter. Please give her to him as his wife.
Context
6Kisha Hamori baba yake Shekemu akaenda kuzungumza na Yakobo. 7Basi wana wa Yakobo walikuwa wamerudi kutoka mashambani mara tu waliposikia kilichotokea. Walikuwa wamejawa na huzuni na ghadhabu, kwa sababu Shekemu alikuwa amefanya jambo la aibu katika Israeli kwa kukutana kimwili na binti wa Yakobo, kitu ambacho hakingepasa kufanyika. 8Lakini Hamori akawaambia, “Moyo wa mwanangu Shekemu umeelekea kwa binti yenu. Tafadhali mpeni awe mke wake. 9Oaneni na sisi, tupeni binti zenu, nanyi mchukue binti zetu. 10Mwaweza kuishi katikati yetu, nchi ni wazi kwenu. Ishini ndani yake, fanyeni biashara humu na mjipatie mali.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.