Mwanzo 33:3
Genesis 33:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Yeye mwenyewe akatangulia mbele na kusujudu mara saba alipomkaribia ndugu yake.
Genesis 33:3 in English
Genesis 33:3 · Berean Standard Bible
But Jacob himself went on ahead and bowed to the ground seven times as he approached his brother.
Context
1Yakobo akainua macho akamwona Esau akija na watu wake 400, kwa hiyo akawagawanya watoto kati ya Lea, Raheli na wale watumishi wake wawili wa kike. 2Akawaweka wale watumishi wa kike na watoto wao mbele, Lea na watoto wake wakafuata, Raheli na Yosefu wakaja nyuma. 3Yeye mwenyewe akatangulia mbele na kusujudu mara saba alipomkaribia ndugu yake. 4Lakini Esau akamkimbilia Yakobo kumlaki na kumkumbatia, akamwangukia shingoni na kumbusu. Nao wakalia. 5Esau akainua macho akawaona wale wanawake na watoto. Akauliza, “Hawa uliofuatana nao ni nani?”
Yakobo akamjibu, “Ni watoto ambao Mungu amempa mtumishi wako kwa neema.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.