Mwanzo 33:2
Genesis 33:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Akawaweka wale watumishi wa kike na watoto wao mbele, Lea na watoto wake wakafuata, Raheli na Yosefu wakaja nyuma.
Genesis 33:2 in English
Genesis 33:2 · Berean Standard Bible
He put the maidservants and their children in front, Leah and her children next, and Rachel and Joseph at the rear.
Context
1Yakobo akainua macho akamwona Esau akija na watu wake 400, kwa hiyo akawagawanya watoto kati ya Lea, Raheli na wale watumishi wake wawili wa kike. 2Akawaweka wale watumishi wa kike na watoto wao mbele, Lea na watoto wake wakafuata, Raheli na Yosefu wakaja nyuma. 3Yeye mwenyewe akatangulia mbele na kusujudu mara saba alipomkaribia ndugu yake. 4Lakini Esau akamkimbilia Yakobo kumlaki na kumkumbatia, akamwangukia shingoni na kumbusu. Nao wakalia.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.