Native Bible

Genesis 33:18 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Baada ya Yakobo kutoka Padan-Aramu, alifika salama katika mji wa Shekemu huko Kanaani na kuweka kambi yake karibu na mji.

Genesis 33:18 in English

Genesis 33:18 · Berean Standard Bible

After Jacob had come from Paddan-aram,* he arrived safely at the city of Shechem in the land of Canaan, and he camped just outside the city.

Context

16Hivyo siku hiyo Esau akashika njia akarudi Seiri. 17Pamoja na hayo, Yakobo akaenda Sukothi,* mahali alipojijengea makazi kwa ajili yake na mabanda kwa ajili ya mifugo yake. Hii ndiyo sababu sehemu ile inaitwa Sukothi. 18Baada ya Yakobo kutoka Padan-Aramu, alifika salama katika mji wa Shekemu huko Kanaani na kuweka kambi yake karibu na mji. 19Akanunua kiwanja kutoka kwa wana wa Hamori, baba wa Shekemu, kwa bei ya vipande mia vya fedha, ambapo alipiga hema lake. 20Pale akajenga madhabahu na kupaita El-Elohe-Israeli.*

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.