Native Bible

Genesis 33:17 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Pamoja na hayo, Yakobo akaenda Sukothi,* mahali alipojijengea makazi kwa ajili yake na mabanda kwa ajili ya mifugo yake. Hii ndiyo sababu sehemu ile inaitwa Sukothi.

Genesis 33:17 in English

Genesis 33:17 · Berean Standard Bible

but Jacob went on to Succoth,* where he built a house for himself and shelters for his livestock; that is why the place was called Succoth.

Context

15Esau akamwambia, “Basi na niwaache baadhi ya watu wangu pamoja nawe.” Yakobo akauliza, “Lakini kwa nini ufanye hivyo, niache tu nipate kibali machoni pa bwana wangu.” 16Hivyo siku hiyo Esau akashika njia akarudi Seiri. 17Pamoja na hayo, Yakobo akaenda Sukothi,* mahali alipojijengea makazi kwa ajili yake na mabanda kwa ajili ya mifugo yake. Hii ndiyo sababu sehemu ile inaitwa Sukothi. 18Baada ya Yakobo kutoka Padan-Aramu, alifika salama katika mji wa Shekemu huko Kanaani na kuweka kambi yake karibu na mji. 19Akanunua kiwanja kutoka kwa wana wa Hamori, baba wa Shekemu, kwa bei ya vipande mia vya fedha, ambapo alipiga hema lake.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.