Native Bible

Genesis 32:27 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Yule mtu akamuuliza, “Jina lako nani?” Akajibu, “Yakobo.”

Genesis 32:27 in English

Genesis 32:27 · Berean Standard Bible

“What is your name?” the man asked. “Jacob,” he replied.

Context

25Yule mtu alipoona kuwa hawezi kumshinda, aligusa kiungio cha nyonga ya Yakobo kwa hiyo nyonga yake ikateguka wakati alipokuwa akishikana mweleka na yule mtu. 26Ndipo yule mtu akasema, “Niache niende, kwa kuwa ni mapambazuko.” Lakini Yakobo akajibu, “Sitakuacha uende usiponibariki.” 27Yule mtu akamuuliza, “Jina lako nani?” Akajibu, “Yakobo.” 28Ndipo yule mtu akasema, “Jina lako halitakuwa tena Yakobo, bali Israeli,* kwa sababu umeshindana na Mungu na watu pia, nawe umeshinda.” 29Yakobo akasema, “Tafadhali niambie jina lako.” Lakini akajibu, “Kwa nini kuniuliza Jina langu?” Ndipo akambariki huko.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.