Native Bible

Genesis 32:26 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Ndipo yule mtu akasema, “Niache niende, kwa kuwa ni mapambazuko.” Lakini Yakobo akajibu, “Sitakuacha uende usiponibariki.”

Genesis 32:26 in English

Genesis 32:26 · Berean Standard Bible

Then the man said, “Let me go, for it is daybreak.” But Jacob replied, “I will not let you go unless you bless me.”

Context

24Kwa hiyo Yakobo akaachwa peke yake na mtu mmoja akashikana naye mweleka mpaka mapambazuko. 25Yule mtu alipoona kuwa hawezi kumshinda, aligusa kiungio cha nyonga ya Yakobo kwa hiyo nyonga yake ikateguka wakati alipokuwa akishikana mweleka na yule mtu. 26Ndipo yule mtu akasema, “Niache niende, kwa kuwa ni mapambazuko.” Lakini Yakobo akajibu, “Sitakuacha uende usiponibariki.” 27Yule mtu akamuuliza, “Jina lako nani?” Akajibu, “Yakobo.” 28Ndipo yule mtu akasema, “Jina lako halitakuwa tena Yakobo, bali Israeli,* kwa sababu umeshindana na Mungu na watu pia, nawe umeshinda.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.