Mwanzo 32:24
Genesis 32:24 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa hiyo Yakobo akaachwa peke yake na mtu mmoja akashikana naye mweleka mpaka mapambazuko.
Genesis 32:24 in English
Genesis 32:24 · Berean Standard Bible
So Jacob was left all alone, and there a man * wrestled with him until daybreak.
Context
22Usiku ule Yakobo akaamka akawachukua wake zake wawili, watumishi wake wawili wa kike na wanawe kumi na mmoja na akavuka kivuko cha Yaboki. 23Baada ya kuwavusha ngʼambo ya kijito, alivusha pia mali zake zote. 24Kwa hiyo Yakobo akaachwa peke yake na mtu mmoja akashikana naye mweleka mpaka mapambazuko. 25Yule mtu alipoona kuwa hawezi kumshinda, aligusa kiungio cha nyonga ya Yakobo kwa hiyo nyonga yake ikateguka wakati alipokuwa akishikana mweleka na yule mtu. 26Ndipo yule mtu akasema, “Niache niende, kwa kuwa ni mapambazuko.”
Lakini Yakobo akajibu, “Sitakuacha uende usiponibariki.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.