Native Bible

Genesis 31:48 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Labani akasema, “Lundo hili ni shahidi kati yako na mimi leo.” Ndiyo maana likaitwa Galeedi.

Genesis 31:48 in English

Genesis 31:48 · Berean Standard Bible

Then Laban declared, “This mound is a witness between you and me this day.” Therefore the place was called Galeed.

Context

46Akawaambia jamaa yake, “Kusanyeni mawe.” Hivyo wakachukua mawe na kuyakusanya yakawa lundo, wakala chakula hapo karibu na hilo lundo. 47Labani akaliita Yegar-Sahadutha* na Yakobo akaliita Galeedi.* 48Labani akasema, “Lundo hili ni shahidi kati yako na mimi leo.” Ndiyo maana likaitwa Galeedi. 49Pia liliitwa Mispa,* kwa sababu alisema, “Bwana na aweke ulinzi kati yako na mimi wakati kila mmoja akiwa mbali na mwingine. 50Kama ukiwatenda mabaya binti zangu au ukioa wake wengine zaidi ya binti zangu, hata ingawa hakuna hata mmoja aliye pamoja nasi, kumbuka kwamba Mungu ni shahidi kati yako na mimi.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.