Mwanzo 27:8
Genesis 27:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Sasa, mwanangu, nisikilize kwa makini na ufanye yale ninayokuambia:
Genesis 27:8 in English
Genesis 27:8 · Berean Standard Bible
Now, my son, listen to my voice and do exactly as I tell you.
Context
6Rebeka akamwambia Yakobo mwanawe, “Tazama, nimemsikia baba yako akimwambia ndugu yako Esau, 7‘Niletee mawindo, kisha ukaniandalie chakula kitamu nile, ili niweze kukubariki mbele za Bwana kabla sijafa.’ 8Sasa, mwanangu, nisikilize kwa makini na ufanye yale ninayokuambia: 9Nenda sasa katika kundi ukaniletee wana-mbuzi wawili wazuri, ili niandalie chakula kitamu kwa ajili ya baba yako, kama vile anavyopenda. 10Kisha umpelekee baba yako ale, ili apate kukubariki kabla hajafa.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.