Native Bible

Genesis 27:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

‘Niletee mawindo, kisha ukaniandalie chakula kitamu nile, ili niweze kukubariki mbele za Bwana kabla sijafa.’

Genesis 27:7 in English

Genesis 27:7 · Berean Standard Bible

‘Bring me some game and prepare me a tasty dish to eat, so that I may bless you in the presence of the LORD before I die.’

Context

5Basi Rebeka alikuwa akisikiliza Isaki alipokuwa akizungumza na mwanawe Esau. Esau alipoondoka kwenda nyikani kuwinda nyama pori na kuleta, 6Rebeka akamwambia Yakobo mwanawe, “Tazama, nimemsikia baba yako akimwambia ndugu yako Esau, 7‘Niletee mawindo, kisha ukaniandalie chakula kitamu nile, ili niweze kukubariki mbele za Bwana kabla sijafa.’ 8Sasa, mwanangu, nisikilize kwa makini na ufanye yale ninayokuambia: 9Nenda sasa katika kundi ukaniletee wana-mbuzi wawili wazuri, ili niandalie chakula kitamu kwa ajili ya baba yako, kama vile anavyopenda.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.