Mwanzo 27:39
Genesis 27:39 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Baba yake Isaki akamjibu, akamwambia, “Makao yako yatakuwa mbali na utajiri wa dunia, mbali na umande wa mbinguni juu.
Genesis 27:39 in English
Genesis 27:39 · Berean Standard Bible
His father Isaac answered him: “Behold, your dwelling place shall be away from the richness of the land, away from the dew of heaven above.
Context
37Isaki akamjibu Esau, “Nimemfanya yeye kuwa bwana juu yako, pia nimewafanya ndugu zako wote kuwa watumishi wake, nimemtegemeza kwa nafaka na divai mpya. Sasa nitaweza kukufanyia nini, mwanangu?” 38Esau akamwambia baba yake, “Je, baba yangu una baraka moja tu? Unibariki mimi pia, baba yangu!” Kisha Esau akalia kwa sauti kubwa. 39Baba yake Isaki akamjibu, akamwambia,
“Makao yako yatakuwa
mbali na utajiri wa dunia,
mbali na umande wa mbinguni juu. 40Utaishi kwa upanga,
nawe utamtumikia ndugu yako,
lakini wakati utakapokuwa umejikomboa,
utatupa nira yake
kutoka shingoni mwako.” 41Esau akawa na kinyongo dhidi ya Yakobo kwa ajili ya baraka ambazo baba yake alikuwa amembariki. Akasema moyoni mwake, “Siku za kuomboleza kwa ajili ya baba yangu zimekaribia, ndipo nitamuua ndugu yangu Yakobo.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.