Mwanzo 27:38
Genesis 27:38 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Esau akamwambia baba yake, “Je, baba yangu una baraka moja tu? Unibariki mimi pia, baba yangu!” Kisha Esau akalia kwa sauti kubwa.
Genesis 27:38 in English
Genesis 27:38 · Berean Standard Bible
Esau said to his father, “Do you have only one blessing, my father? Bless me too, O my father!” Then Esau wept aloud.
Context
36Esau akasema, “Si ndiyo sababu anaitwa Yakobo? Amenidanganya mara hizi mbili: Alichukua haki yangu ya kuzaliwa na sasa amechukua baraka yangu!” Kisha akauliza, “Hukubakiza hata baraka moja kwa ajili yangu?” 37Isaki akamjibu Esau, “Nimemfanya yeye kuwa bwana juu yako, pia nimewafanya ndugu zako wote kuwa watumishi wake, nimemtegemeza kwa nafaka na divai mpya. Sasa nitaweza kukufanyia nini, mwanangu?” 38Esau akamwambia baba yake, “Je, baba yangu una baraka moja tu? Unibariki mimi pia, baba yangu!” Kisha Esau akalia kwa sauti kubwa. 39Baba yake Isaki akamjibu, akamwambia,
“Makao yako yatakuwa
mbali na utajiri wa dunia,
mbali na umande wa mbinguni juu. 40Utaishi kwa upanga,
nawe utamtumikia ndugu yako,
lakini wakati utakapokuwa umejikomboa,
utatupa nira yake
kutoka shingoni mwako.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.