Mwanzo 26:11
Genesis 26:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hivyo Abimeleki akatoa amri kwa watu wote, akisema, “Yeyote atakayemnyanyasa mtu huyu au mkewe hakika atauawa.”
Genesis 26:11 in English
Genesis 26:11 · Berean Standard Bible
So Abimelech warned all the people, saying, “Whoever harms this man or his wife will surely be put to death.”
Context
9Abimeleki akamwita Isaki akamwambia, “Hakika huyu ni mke wako! Mbona uliniambia, ‘Huyu ni dada yangu?’ ”
Isaki akamjibu, “Kwa sababu nilifikiri ningeweza kuuawa kwa sababu yake.” 10Ndipo Abimeleki akamjibu, “Ni nini hiki ulichotufanyia? Ingewezekana mtu yeyote akawa amekutana kimwili na mke wako, nawe ungeleta hatia juu yetu.” 11Hivyo Abimeleki akatoa amri kwa watu wote, akisema, “Yeyote atakayemnyanyasa mtu huyu au mkewe hakika atauawa.” 12Isaki akapanda mazao katika nchi hiyo, kwa mwaka huo huo, akavuna mara mia, kwa sababu Bwana alimbariki. 13Isaki akawa tajiri, mali zake zikaendelea kuongezeka mpaka akawa tajiri sana.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.