Native Bible

Genesis 24:63 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Isaki akatoka kwenda shambani kutafakari wakati wa jioni, alipoinua macho yake, akaona ngamia wanakuja.

Genesis 24:63 in English

Genesis 24:63 · Berean Standard Bible

Early in the evening, Isaac went out to the field to meditate, and looking up, he saw the camels approaching.

Context

61Rebeka na vijakazi wake wakajiandaa, wakapanda ngamia zao wakafuatana na yule mtu. Hivyo yule mtumishi akamchukua Rebeka akaondoka. 62Basi Isaki alikuwa ametoka Beer-Lahai-Roi, kwa kuwa alikuwa anaishi nchi ya Negebu. 63Isaki akatoka kwenda shambani kutafakari wakati wa jioni, alipoinua macho yake, akaona ngamia wanakuja. 64Rebeka pia akainua macho akamwona Isaki. Akashuka kutoka kwenye ngamia wake 65na akamuuliza yule mtumishi, “Ni nani mtu yule aliye kule shambani anayekuja kutulaki?” Yule mtumishi akajibu, “Huyu ndiye bwana wangu.” Hivyo Rebeka akachukua shela yake akajifunika.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.