Native Bible

Genesis 22:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Basi malaika wa Bwana akamwita Abrahamu kutoka mbinguni mara ya pili,

Genesis 22:15 in English

Genesis 22:15 · Berean Standard Bible

And the angel of the LORD called to Abraham from heaven a second time,

Context

13Abrahamu akainua macho yake, akaona kondoo dume amenaswa pembe zake nyuma yake katika kichaka. Akaenda akamchukua huyo kondoo dume, akamtoa awe sadaka ya kuteketezwa badala ya mwanawe. 14Abrahamu akapaita mahali pale Yehova-Yire.* Mpaka siku ya leo inasemekana, “Katika mlima wa Bwana itapatikana.” 15Basi malaika wa Bwana akamwita Abrahamu kutoka mbinguni mara ya pili, 16akasema, “Ninaapa kwa nafsi yangu, asema Bwana, kwamba kwa sababu umefanya jambo hili na hukunizuilia mwanao, mwana wako wa pekee, 17hakika nitakubariki, na nitauzidisha uzao wako kama nyota za angani na kama mchanga ulioko pwani. Wazao wako watamiliki miji ya adui zao,

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.