Mwanzo 22:13
Genesis 22:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Abrahamu akainua macho yake, akaona kondoo dume amenaswa pembe zake nyuma yake katika kichaka. Akaenda akamchukua huyo kondoo dume, akamtoa awe sadaka ya kuteketezwa badala ya mwanawe.
Genesis 22:13 in English
Genesis 22:13 · Berean Standard Bible
Then Abraham looked up and saw behind him a ram * in a thicket, caught by its horns. So he went and took the ram and offered it as a burnt offering in place of his son.
Context
11Lakini malaika wa Bwana akamwita kutoka mbinguni, akamwambia, “Abrahamu! Abrahamu!”
Akajibu, “Mimi hapa.” 12Akamwambia, “Usimdhuru kijana, wala usimtendee jambo lolote. Sasa ninajua kwamba unamcha Mungu, kwa sababu hukunizuilia mwanao, mwana wako wa pekee.” 13Abrahamu akainua macho yake, akaona kondoo dume amenaswa pembe zake nyuma yake katika kichaka. Akaenda akamchukua huyo kondoo dume, akamtoa awe sadaka ya kuteketezwa badala ya mwanawe. 14Abrahamu akapaita mahali pale Yehova-Yire.* Mpaka siku ya leo inasemekana, “Katika mlima wa Bwana itapatikana.” 15Basi malaika wa Bwana akamwita Abrahamu kutoka mbinguni mara ya pili,
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.