Mwanzo 22:12
Genesis 22:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Akamwambia, “Usimdhuru kijana, wala usimtendee jambo lolote. Sasa ninajua kwamba unamcha Mungu, kwa sababu hukunizuilia mwanao, mwana wako wa pekee.”
Genesis 22:12 in English
Genesis 22:12 · Berean Standard Bible
“Do not lay a hand on the boy or do anything to him,” said the angel, “for now I know that you fear God, since you have not withheld your only son from me.*”
Context
10Kisha akanyoosha mkono wake na akachukua kisu ili amchinje mwanawe. 11Lakini malaika wa Bwana akamwita kutoka mbinguni, akamwambia, “Abrahamu! Abrahamu!”
Akajibu, “Mimi hapa.” 12Akamwambia, “Usimdhuru kijana, wala usimtendee jambo lolote. Sasa ninajua kwamba unamcha Mungu, kwa sababu hukunizuilia mwanao, mwana wako wa pekee.” 13Abrahamu akainua macho yake, akaona kondoo dume amenaswa pembe zake nyuma yake katika kichaka. Akaenda akamchukua huyo kondoo dume, akamtoa awe sadaka ya kuteketezwa badala ya mwanawe. 14Abrahamu akapaita mahali pale Yehova-Yire.* Mpaka siku ya leo inasemekana, “Katika mlima wa Bwana itapatikana.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.