Native Bible

Genesis 22:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kisha akanyoosha mkono wake na akachukua kisu ili amchinje mwanawe.

Genesis 22:10 in English

Genesis 22:10 · Berean Standard Bible

Then Abraham reached out his hand and took the knife to slaughter his son.

Context

8Abrahamu akajibu, “Mwanangu, Mungu mwenyewe atajipatia mwana-kondoo kwa ajili ya hiyo sadaka ya kuteketezwa.” Nao hawa wawili wakaendelea mbele pamoja. 9Walipofika mahali pale alipokuwa ameambiwa na Mungu, Abrahamu akajenga madhabahu hapo, akaziweka kuni juu yake. Akamfunga Isaki mwanawe na akamlaza kwenye madhabahu, juu ya zile kuni. 10Kisha akanyoosha mkono wake na akachukua kisu ili amchinje mwanawe. 11Lakini malaika wa Bwana akamwita kutoka mbinguni, akamwambia, “Abrahamu! Abrahamu!” Akajibu, “Mimi hapa.” 12Akamwambia, “Usimdhuru kijana, wala usimtendee jambo lolote. Sasa ninajua kwamba unamcha Mungu, kwa sababu hukunizuilia mwanao, mwana wako wa pekee.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.