Mwanzo 20:15
Genesis 20:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Abimeleki akasema, “Nchi yangu iko mbele yako, ishi popote unapotaka.”
Genesis 20:15 in English
Genesis 20:15 · Berean Standard Bible
And Abimelech said, “Look, my land is before you. Settle wherever you please.”
Context
13Wakati Bwana aliponifanya nisafiri mbali na nyumbani mwa baba yangu, nilimwambia, ‘Hivi ndivyo utakavyoonyesha pendo lako kwangu: Kila mahali tutakapokwenda, kuhusu mimi sema, “Huyu ni kaka yangu.” ’ ” 14Kisha Abimeleki akatwaa kondoo na ngʼombe, na watumwa wa kiume na wa kike akampa Abrahamu, akamrudisha Sara kwa mumewe. 15Abimeleki akasema, “Nchi yangu iko mbele yako, ishi popote unapotaka.” 16Akamwambia Sara, “Ninampa kaka yako shekeli elfu moja za fedha. Hii ni kufidia kosa lililofanyika dhidi yako mbele ya wote walio pamoja nawe; haki yako imethibitishwa kabisa.” 17Kisha Abrahamu akamwomba Mungu, naye Mungu akamponya Abimeleki, mke wake, na watumwa wake wa kike kwamba waweze kupata watoto tena,
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.